Week 13 Guide: Juma 13
Loading...
Authors
Alexander, Andy, S.J.
Waldron, Maureen McCann
Issue Date
2000-01-01
Type
Text
Language
en_US
Keywords
Alternative Title
Abstract
JUMA LA KUMI NA TATU|Mungu Anatayarisha Njia|Mwongozo: Ahadi|Kurasa za mwanzo za Kitabu cha Picha cha Yesu (Albamu ya Picha) kinatuonyesha ustahamilivu na uaminifu wa Mungu katika matayarisho ya kumtuma Yesu Kristu kuja kuwa nasi. Tunaweza kumwona Mungu akiwaita Abrahamu na Sara na kuwaelekeza waihame nchi yao, na kuanza safari mpya ya maisha. Tunaona pia kuzaliwa kwa Isaka ya Yakobo (Israeli). Kitabu hiki cha picha kina kurasa nyingi za maisha ya Waisraeli: Utumwani Misri, kuzaliwa na maisha ya Musa, mpango wa Mungu wa ‘Kutoka’ na Ukombozi wa wana wa Israeli kutoka katika mikono ya Farao na Wamisri, miaka arobaini ya Waisraeli jangwani, na miaka ya mwanzo katika Nchi ya Ahadi.|Mungu aliteua watu kuwa waamuzi baina ya watu, na kisha akawateua wafalme kuongoza watu wake, na tena akawatuma manabii kuwakosoa na kuwashauri watu na wafalme wao hasa pale walipopotoka. Tunakanganywa, tunapigwa na butwaa na hata kupata mshtuko mkubwa tunapoona jinsi watu wateule wa Mungu wanavyokosa uaminifu kwa Mungu, jinsi taifa lao linavyogawanyika, na jinsi haya yanavyowangoza kuangukia katika utumwa kwa Wababeli. Baada tunawaona wakilijenga tena Hekalu la Mungu, wanapata tena uhuru wao na kuishi kwa amani ya kiasi, chini ya himaya ya Warumi.|Maandiko Matakatifu:|Mwanzo 12:1-7|Mwanzo 18:1-15|Mwanzo 37:1-36|Kutoka 2:1-25|Kutoka 15:1-18|Zaburi 81
Description
Citation
Publisher
Creighton University, Online Ministries