Week 17 Guide: Juma 17

Loading...
Thumbnail Image

Authors

Alexander, Andy, S.J.
Waldron, Maureen McCann

Issue Date

2000-01-01

Type

Text

Language

en_US

Keywords

Research Projects

Organizational Units

Journal Issue

Alternative Title

Abstract

Tumeanza kutafakari maisha ya Yesu. Tumeona jinsi, tangu hapo katika awali utoto wake, maisha yake yalijengeka katika kumtumainia Mungu, kujisalimisha katika mpango wa Mungu, na kukubali hali ya umaskini na kukataliwa. Tumekuwa tukisali ili kumjua, kumpenda na kuwa naye kwa undani zaidi. Kabla hatujaendelea mbele kutafakari jinsi alivyotekeleza mwito wake mbele za watu, tunatenga majuma machache kujiweka katika hali ambayo mafungo haya yatakuwa na nguvu ya kuyagusa kwa ndani kabisa maisha yetu na kuyaekeza maamuzi tutakayokuwa tukifanya tutakapokuwa tunamkaribia zaidi Yesu.|Ni shauku ambayo hutuongoza katika kuchagua au kuamua. Kuelewa maamuzi na chaguzi tunazofanya, na kujitayarisha kufanya maamuzi mapya, sharti tuzielewe shauku zetu na kuwa tayari kuzirekebisha ikibidi.|Juma lote hili, katika muda unaopata baada ya kumaliza shughuli fulani na kabla hujaanza nyingine, au uwapo katika kwenda sehemu ya shughuli inayofuata, au ukiwa katika mapumziko mafupi katika siku ambapo umebanwa sana na shughuli jaribu kuelewa jinsi ya kuwa na shauku au kiu inayotuweka pamoja na Yesu. Huku tukijifunza kuikubali njia ya Yesu kwa uhuru, tutajaribu kuelewa nini hasa ni kinyume cha kuwa na shauku, njia ambayo tunaweza kusema inazinga tamaduni zetu mamboleo.|Maandiko Matakatifu:|Matayo 5:1-16|Wagalatia 5:16-26|Wafilipi 4:11-15|1 Timoteo 6:6-10, 17-19|1 Petro 5:1-11

Description

Citation

Publisher

Creighton University, Online Ministries

License

Journal

Volume

Issue

PubMed ID

DOI

ISSN

EISSN