Week 16 Guide: Juma 16

Loading...
Thumbnail Image

Authors

Alexander, Andy, S.J.
Waldron, Maureen McCann

Issue Date

2000-01-01

Volume

Issue

Type

Text

Language

en_US

Keywords

Research Projects

Organizational Units

Journal Issue

Alternative Title

Abstract

JUMA LA KUMI NA SITA|Maisha Nje ya Hadhara kwa Miaka Thelathini|Mwongozo: Mwana wa Seremala|Mojawapo ya ukweli wa kushangaza sana kumhusu Yesu Kristu ni kuwa tunajua kidogo sana kuhusu maisha yake katika miaka thelathini ya mwanzo wa maisha yake. Tunajua alipoanza kazi yake hadharani, wali walimjua yeye na ndugu zake walishangazwa sana. Kwa dharau wengine walitoa mashambulio yao dhidi yake wakisemezana: “huyu siye yule mwana wa seremala?”|Juma hili la mafungo linatupa muda wa kumjua Yesu anayekua katika ubinadamu wake (anayeongezeka umri). Kwa kuwa kuna Maandiko machache sana ya kurejea kuhusu maisha yake kati ya kuzaliwa kwake na kubatizwa kwake, tutatumia ubunifu wetu kujazia sehemu zile ambazo hatuambiwi mengi na maandiko—ila tunajua kweli mbalimbali za historia ya wakati huo, kazi ya baba yake, imani na tamaduni za watu wake, n.k. Zaidi, kama tukiifikiria hali ya utu-uzima ambayo Yesu alifikia, tunaweza pia kutafakari jinsi utoto wake ulivyokuwa, alikuwa mtoto wa namna gani, mambo gani alipambana nayo katika maisha na fikara, ni maamuzi gani hasa alifanya, n.k. Kwa kutumia kile tunachojua kuhusu maendeleo ya watoto hadi kufikia ujana, halafu kufikia utu uzima, tunaweza kufanya ubunifu mzuri kuhusu mambo kadhaa ya kibinadamu ambayo sharti Yesu aliyakabili. Tukisali namna hii tuingie katika zoezi la kumjua kwa undani zaidi, ili kwamba tuweze kumpenda zaidi na kufikia shauku yetu ya ndani kabisa ya kuwa naye katika utume wake aliopewa na Mungu Baba.|Maandiko Matakatifu|Luka 2:22-38|Luka 2:39-40|Luka 2:41-52|Waebrania 1:1-2

Description

Citation

Publisher

Creighton University, Online Ministries

License

Journal

Volume

Issue

PubMed ID

DOI

Identifier

Additional link

ISSN

EISSN