Week 10 Guide: Juma 10

Loading...
Thumbnail Image

Authors

Alexander, Andy, S.J.
Waldron, Maureen McCann

Issue Date

2000-01-01

Type

Text

Language

en_US

Keywords

Research Projects

Organizational Units

Journal Issue

Alternative Title

Abstract

JUMA LA KUMI|Mwaliko wa Kupenda — Ambatana Nami Tafadhali|Mwongozo: Wito wa Ubatizo Wetu|Jaribu kuwaza kama vile rafiki yako karudi sasa hivi kutoka katika nchi iliyo na umaskini na matatizo yanayokithiri; nchi ambapo wengi hufa kwa vita, ukosefu wa chakula na magonjwa ya kila namna. Jaribu kuwaza mwito atakaokufikishia:|Rafiki yangu, niliyoshuhudia yamebadilisha maisha yangu kabisa. Moyo wangu bado unaguswa na mtoto mdogo niliyemkuta katika wodi ya watoto katika hospitali. Nasikia mwito kutoka ndani kabisa moyoni kurudi tena katika nchi hiyo na kujitolea kusaidia maskini ingalao kwa mwaka mmoja. Kama mimi na wewe tukipata nafasi ya kuweza kwenda huko, utakuwa tayari kuambatana nami tafadhali? Najua mimi na wewe tunaweza kufanya kazi pamoja kutenda jambo la kuwafaa maskini hawa. Katika kutenda kazi nitahitaji sana upendo wako kutiwa moyo na kuungwa mkono na wewe. Hakika nakuhitaji. Najua kuwa haitakuwa kazi rahisi kila wakati, lakini tukiwa pamoja bega kwa bega, hakika hatutalemewa kiasi cha kushindwa. Na najua dhahiri ni kwa kiasi gani tukifanya kazi pamoja kusaidia wengine kutaongeza upendo baina yetu, pale tutakapoona tunakamilisha jambo la taadhima pamoja. Tafadhali ambatana nami.|Katika juma hili zima, tutakuwa tukitafakari nguvu ya mwito huu kama vile umetoka kwa mtu tumpendaye hasa. Utakuwa na matokeo au athari gani kwangu? Kama huyu ni mtu nimpendaye, vitisho vya hali ngumu ambayo inaweza kutukabili katika kutoa msaada inaweza kutukatisha tamaa tuuweke pembeni mpango huu? Vilevile katika juma hili tutalinganisha mwito huo na mwaliko tuupokeao kutoka kwa Yesu Kristu:|Katika majuma kadhaa yaliyopita, imekuwa furaha niliyokuwa nikiitamani—kukuonyesha wazi wazi jinsi ninavyokupenda. Hakika ni kwa kiasi kikubwa sana nilipenda wewe utambue shauku yangu kubwa ya kuiweka huru roho yako. Na sasa kwa kuwa umeniomba nikufunulie ni jinsi gani waweza kuyaitikia mapendo yangu kwako, najawa na shauku ya kukualika uambatane nami.|Maandiko Matakatifu|Luka 4:14-20|Marko 1:16-20|Luka 5:27-31|Luka 9:57-62|Luka 12:32-34

Description

Citation

Publisher

Creighton University, Online Ministries

License

Journal

Volume

Issue

PubMed ID

DOI

ISSN

EISSN