Nitaanzaje Kufanya Mafungo Haya? (How Do I Get Started Making the Retreat)

Loading...
Thumbnail Image
Authors
Alexander, Andy, S.J.
Waldron, Maureen McCann
Issue Date
2000-01-01
Type
Text
Language
en_US
Keywords
Research Projects
Organizational Units
Journal Issue
Alternative Title
Abstract
Kila Juma la mafungo lina Ukurasa Mwongozo ambao huelekeza jinsi ya kufanya mafungo katika juma hilo. Ukurasa Mwongozo unatoa mada ya wiki husika, hususan neema ya kusalia (kuomba) katika juma hilo. Kwenye upande wa kulia wa Ukurasa Mwongozo wa kila juma kumewekwa zana za kukusaidia katika juma hilo.|Picha: Hii hutupa mwelekeo au shabaha ya juma husika. Kuna maelekezo hapo kuhusiana na kuiweka picha hiyo kama taswira ya mbele ya kompyuta yako(tarakilishi yako). Hatua ya Kwanza: Hapa pana mwongozo zaidi kwa ajili ya kuanza juma husika na kutoa mtazamo sahihi wa tafakari katika juma la mafungo.|Mkoba wa Safari: Padre Larry Gillick, S.J. huandika tafakari yake fupi ya juma hilo kama usaidizi wa kuingia na kuenenda vema katika safari hii ya kiroho.|Katika Maneno Haya au Mengine Yanayofanana Nayo: Msaada katika kusali kwa lugha na maneno yangu mwenyewe. Hapa nakaribishwa kuwa na mtazamo sahihi wa mafungo kama sala yangu.|Kusoma: Kusoma Maandiko Matakatifu au machapisho mengine yanisaidiayo kuomba neema ya wiki husika.|Sala: Hiki ni chanzo kikuu cha kustawisha tafakari katika juma la mafungo.
Description
Citation
Publisher
Creighton University, Online Ministries
License
Journal
Volume
Issue
PubMed ID
DOI
ISSN
EISSN