Week 15 Guide: Juma 15
Loading...
Authors
Alexander, Andy, S.J.
Waldron, Maureen McCann
Issue Date
2000-01-01
Type
Text
Language
en_US
Keywords
Alternative Title
Abstract
JUMA LA KUMI NA TANO|Kazaliwa Kwetu, Kwa Ajili Yetu|Mwongozo: Neema ya Kuzaliwa Kwake|Akinamama wengi, katika kusherehekea siku ya kuzaliwa ya watoto wao, huwasimulia kwa kwa uyakinifu yaliyotokea siku na wakati walipozaliwa. Mwaka hadi mwaka, simulizi hizi hurudiwa. Katika muda huu wa mafungo yako, tunampa Yesu nafasi atupe simulizi ya kuzaliwa kwake. Hii itatubidi twende mbele zaidi ya simulizi tunazopata katika Injili kama zilivyoandikwa na Matayo na Luka. Tutaingia ndani kabisa ya simulizi kuliko tafakari zetu za kuzaliwa kwa Yesu Kristu. Juma hili tutapokea neema ya kushuhudia kuzaliwa kwa Yesu na kuelewa maana yake hasa na umuhimu wake kwetu.|Uchu wetu unaendelea. Ni lazima kwetu kuiamsha upya kiu hii ndani yetu katika juma hili, (iwapo imefifia)—kiu au uchu wa kumjua Yesu kwa undani zaidi. Kwa kumwangalia na kumwelewa, tunategemea upendo wetu kwake kuwa mkamilifu zaidi. Upendo wetu kwake unavyoongezeka katika ukamilifu, tunapata uhiari mkubwa zaidi wa kuwa naye katika utume wake.|Maandiko Matakatifu:|Matayo 1:18-24|Luka 2:1-21|Matayo 2:1-12|Matayo 2:13-23|Zaburi 98
Description
Citation
Publisher
Creighton University, Online Ministries