The Week 2 Guide: Juma 2
Loading...
Authors
Alexander, Andy, S.J.
Waldron, Maureen McCann
Issue Date
2000-01-01
Volume
Issue
Type
Text
Language
en_US
Keywords
Alternative Title
Abstract
JUMA LA PILI|Hadithi ya Maisha Yetu: Kuingia Zaidi Ndani Yake|Mwongozo: Kuangalia kwa Makini Zaidi Hadithi za Maisha Yetu|
Kama tulivyopitia “kitabu cha picha” cha hadithi za maisha yetu wiki iliyopita, zimetujia kumbukumbu ambazo zimetuonyesha uwepo wa Mungu katika safari ya maisha yetu hapa duniani. Zoezi letu juma hili litatusaidia kuingia zaidi ndani ya hadithi za maisha yetu.|Njia mojawapo nzuri ya kupenya ndani zaidi katika hadithi za maisha yetu ni kujiuliza na kujibu maswali yaliyo muhimu. Ni kweli tunaendelea kufanya mafungo haya ya kiroho kwa mtandao kati ya maisha yetu yenye harakati na changamoto nyingi katika juma hili na tutaendelea kuweka taswira fulani katika akili na mioyo yetu iwe “dirisha” kupitia kwalo tunaangalia na kutafakari juma zima, kama vile tulivyofanya katika juma la kwanza (angalia Zana za Kukusaidia Kuanza Juma Hili). Maswali haya muhimu ni rahisi kuyakumbuka na ni muhimu kwa kututayarisha kwa majuma yanayofuata. Kama jinsi Mungu “alivyotuunga pamoja tumboni mwa mama zetu,” kama ituambiavyo Zaburi ya 139, kadhalika matukio mbalimbali na yale tunayotutokea katika maisha yetu huendelea kutufanya kuwa watu tulio leo hii.|Maandiko Matakatifu:|Isaya 49:14-16|Hosea 11:1-4|Zaburi 23
Description
Citation
Publisher
Creighton University, Online Ministries
